Mwaka
2013, vuguvugu la Anaconda lilimsaidia Lady Jaydee si tu kukusanya
mashabiki wengi zaidi, bali pia limempa fedha nyingi mno. Hadi sasa
muimbaji huyo ana zaidi ya likes laki mbili kwenye Facebook na followers
zaidi ya 60,000 kwenye Twitter.
Jaydee akiwa na gari yake mpya, Range Rover Evoque
Zaidi ya tiketi 3,500 zilinunuliwa
kwenye show yake ya mwezi June ya Miaka 13 ya Muziki na kuingiza
takribani shilingi milioni 100. Haikuishia hapo, album yake Nothing But
The Truth ilifanya vizuri na kumfanya kuwa msanii pekee wa Bongo Flava
anayeendelea kufurahia mauzo ya album zake.
Hits zake mbili, Joto Hasira na Yahaya
kutoka kwenye santurui take hiyo, zimebadilisha maisha yake na kumfanya
kuwa mwanamuziki aliyekuwa na show nyingi zaidi mwaka jana. Lady
Jaydee alitumbuiza kwenye karibu show zote za Kili Music Tour ambako
aliiingiza si chini ya shilingi milioni 25.
Mwaka jana pia Lady Jaydee amefanya show
nyingi kubwa ikiwemo ile ya uzinduzi wa filamu ya Lulu, Foolish Age,
show yake kwenye Miss Tanzania 2013, Family Day Show ya Arusha
iliyofanyika Eid Pili, Anaconda Show iliyofanyika Triple A na nyingine
iliyofanyika Snow View Hotel. Akiwa Arusha pia, Lady Jaydee aliuza kopi
za album yake kama njugu pamoja na t-shirt za Anaconda zilizouzwa kwa
shilingi 15,000 kila moja.
June mwaka jana, Lady Jaydee alitumbuiza
kwenye semina ya kuwezesha wanawake kuondokana na njaa na umaskini,
iliyofanyika chini ya mfuko wa fursa sawa kwa wote chini ya mama Anna
Mkapa. Biashara yake ya Nyumbani Lounge, imeendelea kufanya vizuri pia
kwa kupata wateja wengi wanaoenda kupata chakula, vinywaji na burudani
kutoka kwa bendi yake ya Machozi.
Bado anaingiza fedha kupitia udhamini wa
Airtel kwenye show yake ya TV ya Diary of Lady Jaydee. Msanii huyo
ambaye jina lake ni Judith Wambura pia miongoni mwa wasanii 24 wa bara
la Afrika waliochukuliwa kwenye mradi wa Coke Studio Africa wa kampuni
ya Cocacola unaoendelea jijini Nairobi Kenya. Na sasa Lady Jaydee
amekuwa msanii wa Tanzania anayemiliki gari aghali zaidi, Range Rover
Evoque.
“Hakupenda kudisclose mambo ya bei wala wapi alikoinunua,” mume na meneja wa Lady Jaydee, Gadner G Habash ameiambia Bongo5.
“Lakini tunashukuru Mungu kwa baraka
zake na nguvu ya mashabiki wake amefikia hapo. Hiyo ni gari aina ya
Range Rover Evoque. Gari hizi mara nyingi hapa Tanzania kuna wakala
wake kampuni inaitwa CMC Moters, ni moja kati ya magari latest sana,”
amesema Gadner.
Gadner amezitaja sababu za mafanikio ya
Jaydee ni pamoja na ‘karama na fadhila ya mwenyezi Mungu, nguvu
anayoipata kutoka kw mashabiki wa muziki nchini.
“Wamekuwa wakimwamini, wamekuwa
wakimsupport na kwa jinsi hiyo ndio maana amekuwa anapata mafanikio.
Sababu ya tatu ni ile commitment yak wake yeye mwenye kama msanii.
Jaydee ni mtu ambaye ana bidii sana kwenye kazi yake na anapenda sana
muziki. Jambo hili linafanya siku zote awe makini na umakini ule
unampelekea awe na mafanikio kusema ukweli. Kitu kingine ni kwamba ni
mtu ambaye anathamini kesho yaani kama leo tumefanya vizuri, je kesho
itakuaje! Huwa anafikiria sana kutowaangusha mashabiki wa muziki
wanaomsupport.”
Gadner amesema pamoja na kuwa na
biashara yake ya Nyumbani Lounge, Lady Jaydee anatarajia kuongeza zaidi
miradi mingine. “Huyu bado ni mjasiriamali mchanga anayejifunza zaidi
na angependa kufanya biashara nyingi lakini muda ni mdogo. Isipokuwa
kwa mwaka huu alitarajia kufanya kitu kingine kuongeza kama biashara.
Hajawa tayari kusema ni kitu gani lakini mwenyezi Mungu akijaalia heri
na afya mwaka huu kuna biashara nyingine Jaydee ataitambulisha, ukiacha
Nyumbani Lounge na muziki,” Gadner amefafanua.
Akiongelea ushiriki wa Jaydee kwenye
kipindi cha Coke Studio Africa, Gadner amesema Jide amejiongezea
connection kubwa na amejifunza mengi.
“Pamoja na kuestablish mawasiliano
lakini kumekuwa na kujifunza kwa malegend kama Salif Keita na zaidi ya
hapo kumekuwa na kama aina flani ya miradi ya kufanya kazi pamoja na
wasanii waliofika pale. Mzee Salif Keita amemkubalia Jaydee wakati
wowote atakapokuwa tayari aende Mali wakafanye wimbo pamoja. Hali
kadhalika Octopizzo kutoka Kenya tayari wameweka kwenye line wimbo wa
kufanya pamoja na Jaydee na wasanii wengine wa Nigeria akiwemo Waje.
Gadner amesema kwakuwa kufanya kazi na
wasanii wa nje kunahitaji maandalizi ya kutosha, muda muafaka ukifika
Jaydee ataanza kuifutilia miradi hiyo.
Gadner ambaye ni mtangazaji wa Times FM,
ameongeza kuwa kwa mwaka 2014 Lady Jaydee atasikika kwenye kazi
alizoshirikishwa ukiwemo wimbo wa Juma Nature, One, Songa na Nikki
Mbishi, huku pia yeye akiachia wimbo mpya uliotayarishwa na Bob Junior
na kwamba Historia unaopatikana kwenye Nothing But The Truth ni wimbo
wa mwisho kutoka kwenye album hiyo.
Amesema video ya Historia imefanywa na kampuni ya Ogopa na kwa sasa ipo kwenye hatua ya editing.
Kuhusu wimbo mpya, Gadner amesema video yake itaongozwa na muongozaji Mtanzania aishiye Marekani, Hefemi.
“Nafikiri Jaydee alikuwa anataka afanye
kitu cha tofauti na ndio maana akaamua amchukue director ambaye yuko
nje ya Tanzania ili atupe picha na idea tofauti.”