Akiwa mmoja kati ya wanadada wanofanya vizuri sana kwenye Tasnia
hii ya BongoMovies ,Wema Sepetu ni msichana anayetoka kwenye Familia
ya kibalozi ni mtoto wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa
Balozi Isaack Sepetu Ibrahimu.
Wema sepetu alizaliwa mnamo mwaka 1988 katika hospitali ya ST.
Andrew's jijini Dar es Salaam na ni mtoto wa mwisho kuzaliwa katika
familia yao yenye watoto wanne wa kike.
Alipata elimu yake ya primary na sekondari katika shule ya
ACADEMIC INTERNATIONAL iliyopo jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda
Nchini Malaysia kusomea mambo ya biashara za kimataifa katka chuo cha
Limkokwing University.
Wema alianza kuigiza rasmi mwaka 2007 alipoonekana kwenye filamu
ya POINT OF NO RETURN ambapo halicheza kama mke wa jamaa tajiri mchawi
ambaye daima huua wapenzi wake wa kike kama sadaka. Wema alifikiri
angeweza kufa pia lakini aliamua kumwomba Mungu na mwishowe alifanikiwa
kuiokoa familia yake na yeye.
Pamoja na filamu hizi Wema ameigiza kwenye filamu nyingine
nyingi kama Red Valentine, White Maria, Tafrani, Sakata, Crazy Tenant,
Diary, Lerato, Dj Benny and Basilisa zilizompatia umaarufu na mafanikio
makubwa.
Pamoja na kuwa na kipaji cha uigizaji wema pia anakipaji kikubwa
cha kuimba na pia alishawahi kushiriki mashindano ya urembo na
kufanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania mnamo mwaka 2006 na kujipatia
zawadi ya gari aina ya Toyota Rav 4.
