Omotola
IMEKUWA ni jambo la kawaida kabisa kuona ndoa za mastaa zikivunjika. Kashfa za ufuska pamoja na nyingine kadha wa kadha zimekuwa zikitajwa kama sababu za kusambaratika kwa ndoa hizo.
Pamoja na kuwako kwa idadi kubwa ya ndoa za mastaa zinazovunjika, wapo wengine ambao ndoa zao zimekuwa mfano mzuri, unapenda kuwafahamu?
Joke Silva
Ndoa ya mwigizaji Joke Silva ni miongoni mwa ndoa chache za Nollywood zilizoweza kukaa kwenye mstari bila ya mgogoro.
Tofauti na ndoa nyingine za Nollywood, ya kwake imeishi kwa kipindi kirefu bila kuwa na kashfa. Mume wa mwigizaji huyu, Olu Jacobs, ni nguli wa maigizo.
Ndoa yao inatajwa kuwa iliyojawa na furaha na baraka tele. Ndoa hiyo kwa sasa ina miongo mitatu na sasa Joke anaonekana kama kioo kwa wanawake wengi Nigeria hususan vijana.
Henrieta Kosoko
Ndoa ya Henrietta Kosoko nayo pia inatajwa kuwa ya mfano. Licha ya kuwa kwenye ukewenza lakini bado inaonekana kuwa ni ndoa imara kiasi cha kuhusudiwa na watu wengi. Siku zote amekuwa mwaminifu si tu kwa mumewe bali hata kwa jamii inayomzunguka jambo linalochangia kuiweka ndoa hiyo kwenye mstari ulio sawa.
Ngozie Orji
Ngozie Orji, mke wa mwigizaji, Zack Orji, naye anatazamwa kama kioo. Ndoa yao imedumu kwa muda wa miongo miwili sasa.
Katika kipindi hicho wamejaliwa kupata watoto watatu. Kwa Nollywood ndoa yao inatajwa kuwa miongoni mwa ndoa zenye mafanikio makubwa sana.