Stori
kubwa inayoongelewa kuhusu tuzo hizi za BET 2014 ambazo kwenye
kipengele cha tuzo inayotolewa kwa msanii/kikudi cha Afrika Diamond
Platnumz pia alichaguliwa kushiriki, ni tuzo hiyo kutolewa saa kadhaa
kabla ya zile tuzo za wasanii wa Marekani kutolewa…. yani kwa ufupi
hafla ya utoaji wa tuzo hizi haitoi nafasi kwa tuzo ya Afrika.asubuhi
wakati tuzo za kina Chris Brown, Beyonce na wengine wakubwa zinatolewa
saa kadhaa baadae usiku, Waafrika wanawekwa peke yao ila ingekua poa
kama wangekua wanatoa tuzo ya Afrika palepale kama wasanii wa Marekani,
ingesaidia kuunyanyua muziki wa Afrika’
Miongoni
mwa waliotoa yao ya moyoni ya kutofurahishwa na utolewaji huu wa tuzo
ya Afrika kivyake na kutojumuishwa na zile za wasanii wa Marekani ni
msanii Ommy Dimpoz.
