Wanawake wengi wanashindwa kujua wao wanatofautiana na wanaume kwa
hisia na hata mawazo ya mapenzi. Wanaume wana mambo wanayoyapenda kutoka
kwa wake zao hasa katika masuala ya mapenzi. Kwanza wanawake wajue
wanaume wengi wana hisia za haraka za kufanya mapenzi kuliko wanawake.
Mwanaume alivyoumbwa ni kwamba akiona tu mfano mwanamke umevaa kanga
moja au umevaa night dress hiyo inatosha kusisimua. Wapo wanawake
wanaowasisimua waume zao bila wao kujua. Mfano umevaa tu kanga moja au
night dress ndani huna kitu. Kwako ni jambo la kawaida lakini kwa
mwanaume sio la kawaida kwa kukuona hivyo tayari unakuwa umeamsha hisia
zake. Ukimwona anakuja kutaka haki yake usidhani anakusumbua. Ujue
tayari mwenzako alishafiria mbali zamani we huna habari.
Ni
vyema ukawa mwangalifu kujua hisia za mwanaume huyo mumeo kama
inawezekana mpe anachohitaji kwani usipofanya hivyo unamwathiri
kisaikolojia na anaweza kufikiria nje. Wanawake wengi wa nje waliowaweka
waume zenu kiganjani hiyo ndio mbinu wanayotumia. Akiwa na ahadi na
mumeo atamkuta kanga moja au amevaa night dress na kila anachohiji
atapewa haraka tena kwa madoido. Kwanini akitaka hayo hayo kwa mkewe
hapewi je ana kosa gani anapofikiria nje?
NB: Nikisema mpe
mumeo Hitaji lake sina maana Umpe mpaka kinyume na maumbile Ukiona
Mumeo kafikia hapo Huyo Hafai si Mume mwenye Busara huyo na wala
hakutakii mema mkatalie na Umwelimishe madhara ya Tendo la ndoa kinyume
na maumbile.
Mvutie mumeo kwa mwenekano wako:
Mvuto
ni muhimu sana kwa mwanaume. Wanaume wanapenda wanawake wanaowavutia
kihisia. Niwaambie wanawake mlioolewa jueni kumvalia mumeo mavazi
yanayomvutia. Sio vibaya kama nilivyosema hapo juu ukavaa kanga
moja kama upo pamoja nae. Kama nilivyoeleza hapo juu mwanaume anasisimka
kwa kuona. Kwanini avaliwe kanga moja na wanawake wa nje wakati wewe
unaweza kuvaa.
Wanawake jueni hili mnapokuwa karibu na waume
zenu jianchieni Kwa mfano hakuna ubaya wakati mumeo karudi kutoka kazini
akiwa amechoka, wakati unampotengea chakula ukavaa kanga moja au
night dress. Unaweza kuona hilo ni jambo dogo lakini kisaikolojia
utakuwa umefanya jambo kubwa. Hapo hata kama atakuwa ameudhiwa kazini
atasahau na kukuona wewe mpenzi wake.
Usafi panga vitu vyako vya chumbani vizuri:
Jambo hili limekuwa lizizungumzwa sana hadi wengine wanasema mwanamke
usafi. Kisaikolojia mpangalio wa vitu ndani na hasa chumbani kama ni
mbovu unaweza kuathiri hata tendo la ndoa. Kama chumba ni kichafu vitu
havijapangwa vizuri kisaikolojia kunapunguza msisimko wa mapenzi na hata
kumfanya mwenzako achukie kufanya na wewe tendo hilo ukadhani
hakupendi.
Mwanamke tandika kitanda chako vizuri panga chumba
chako tandika shuka nzuri. Siku hizi kuna shuka zina maneno ya mapenzi
nunua hiyo uwe unatandika. Kisaikolojia utamfanya mpenzi wako avutiwe
chumba chako na hata wewe mwenyewe. Mazingira mazuri yatamfanya asisimke
haraka kimapenzi anapokuwa na wewe na hata kuitamana nyumba yake na
kurudi mapema nyumbani.
Jinsi chumba kilivyo rafu ndiyo
wanasakolojia wanasema kunafanya ubongo uwe rafu hata kuchukia. Unaweza
kumwona mwenzako anachukia kumbe ni kutokana na mpangilio mbovu wa
chumba ndio sababu inayomfanya achukie.
Uwe msafi wa mwili:
Sio usafi wa chumba pekee unatosha pia na usafi wa mwili wako ni
muhimu. Niwakumbushe wanawake hakuna kitu kinachowachukiza wanaume kama
mwanamke mchafu. Asiyejipenda. Sio lazima ujirembe sana lakini jitahidi
ukawa msafi. Oga vizuri paka mafuta au lotion yako jipulizie manukato
kidogo yanayomvutia mumeo. Sio lazima utumie gharama kubwa usafi wa
kawaida unatosha na kupaka rotion kuna fanya ngozi ya mwanamke ikawa
laini inayovutia wanaume wanapenda sana wanawake wenye ngozi laini yenye
kuvutia inaleta msisimko mumeo anapokuwa anakuangalia mara kwa mara.
Wanawake wa nje hawana zaidi ya hayo ni hayo hapo juu na mengine ndiyo
wanayotumia kuwaweka waume zenu kiganjani. Usijaribu kwenda kwa mganga
hakuna atakachokusaidia memeo atatoka kama wewe humsisimui, hupangi
vitu vyako vizuri na pia kama unaendekeza uchafu ni rahisi mumeo
kufikiria nje.
Kujiamini kwako iwe ni kwa sababu unajua
‘kumhendo’ mumeo kwa kumpa mapenzi ya kiwango cha juu, kumheshimu,
mjali na kumpatia mambo ya msingi ambayo anastahili kuyapata kutoka
kwako. Ukifanya hivyo utaifanya roho yake imsute kila anapotaka
kukusaliti.
Hiyo ndiyo iwe sababu ya wewe kujiamini na wala
huna sababu ya kujinadi kwa wenzako. Tambua kuwa kuna wanaofikia hatua
ya kuhatarisha maisha yao kwa kutoa ‘mtandao’ wakijua kuwa ni njia ya
kuwashika waume zao kumbe wanajitafutia matatizo makubwa.
Wapo
waliopoteza fedha zao nyingi kwa kwenda kwa waganga ili waume zao
wasifurukute mbele zao lakini imekuwa kazi bure. Shituka leo, anza
kutumia mbinu sahihi za kuishikilia ndoa yako na usijidanganye kwa
kufanya mambo ambayo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
Mwanamke aliyekamilika ni yule anayeuthamini mwili wake, sasa kwa nini
leo hii ukubali ‘kumrukisha ukuta’ mumeo ili kumfanya asiende nje? Kwa
nini utumie fedha zako kwenye kumtafutia limbwata mumeo wakati wewe
mwenyewe ni limbwata tosha?