Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo BONGO. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo BONGO. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 10 Oktoba 2013

AGNESS MASOGANGE AMETUA BONGO KUTOKA AFRIKA KUSINI ..PICHA AKIWA AIRPORT


Ikiwa ni wiki chache toka kesi ya video vixen Agnes Gerald a.k.a Masogange ya kutuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya kuisha kwa kulipa faini nchini Afrika Kusini na kuwa mtu huru, hatimaye jana Jumanne amerejea nyumbani Tanzania.



Kupitia Instagram jana Agnes alipost picha (hapo juu) akiwa uwanja wa ndege na kuandika “am cmng homeeeeeeeee”.

Mwishoni mwa mwezi uliopita (September) mrembo huyo aliachiwa huru pamoja na mdogo wake Melissa Edward ambaye mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, Afrika Kusini ilimuachia huru baada ya kukosa ushahidi wa kumtia hatiani.

Jumatatu, 7 Oktoba 2013

KISOSI AOLEWA: NI YULE ALIYEKUWA ANAIGIZA UTEJA NA KITALE KWENYE JUMBA LA DHAHABU



Msanii wa maigizo nchini, Bahati Abilah ‘Kisosi’, ambaye mara nyingi anaigiza kama teja la kike  wiki iliyopita alifunga ndoa na Muhaji Salim nyumbani kwao Temeke jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali.
Akizungumza na paparazi wa Ijumaa huku akiwa mwenye furaha, Kisosi alisema kuwa anamshukuru sana mumewe huyo kumuoa kwani ni wanaume  wachache wanaoweza kuzikubali kazi za wapenzi wao hususan za kisanii na kufunganao ndoa.
Kisosi aliongeza kuwa, kwa jinsi anavyoigiza kama teja la kike na baadhi ya watu kumchukulia hivyo ingekuwa vigumu kuolewa lakini baada ya mchumba wake kujua ilikuwa kazi kama zingine wamefunga ndoa.


 “Unajua watu wengi sana wanajua mimi ni teja kweli la kike kitu ambacho si kweli, hivyo mwanaume  anayekuona kupitia michezo yako na akakupenda kutoka moyoni kama ilivyotokea kwangu ndiye mwanaume wa kweli na nitadumunaye,” alisema Kisosi.

Ijumaa, 4 Oktoba 2013

mambo ya shilole hayo

 Shabiki akimnyonya maziwa Shilole baada ya kumuita jukwaani ili wacheze wote.
 Shilole akionyesha kulegea baada ya kunyonywa na shabiki wake
 jamaa akifaidi ziwa la Shilole

Jumatatu, 2 Septemba 2013

HAYA NDO YANAYOWAKUTA WATANZANIA WALIOKAMATWA NA MADAWA HUKO CHINA

Stori: Na Mwandishi Wetu
Taifa la China halina mzaha mbele ya biashara haramu ya madawa ya kulevya na kwa kutambua kwamba wanaohusika zaidi ni Waafrika, sasa hivi kila mja mwenye ngozi nyeusi aliyepo nchini humo, anapewa msoto wa nguvu.

Wabongo wanaoishi China, kwa sasa wanahenyeshwa isivyo kawaida katika msako uliopewa jina
na Watanzania kwamba ni Oparesheni Safisha Wauza Unga.
Katika hoteli wanazofikia, vijiwe vyao, barabarani na kadhalika, kote huko wanapewa msoto wa guvu kwa kile kinachoelezwa kuwa Wachina hawana imani tena na Watanzania na Waafrika kwa jumla ama wanaoishi nchini humo au hata wale wanaoingia na kutoka.

“Wazungu wa unga (wafanyabiashara wa madawa ya kulevya) wanatuharibia starehe hapa China, hatuishi kwa amani tena. Mtu unaweza kukaguliwa siku nzima kisa eti wanawatafuta wanaouza unga,” alisema Artides Kimota ambaye ni Mtanzania anayeishi China kwa sasa.

Aliongeza: “Unajua sasa hivi China imekuwa na uingizwaji mkubwa wa madawa ya kulevya. Kwa Serikali ya China hii ni kashfa nzito. Kwa vile wanajua Waafrika ndiyo sababu kuu, sasa hivi kila Mwafrika anapewa msukosuko.

“Kwa kweli ukiwa Mwafrika hapa China ni mateso makubwa sana kwa sasa. Kuna agizo la serikali ambalo limelitaka jeshi la polisi hapa China kuhakikisha madawa ya kulevya yanatokomezwa na wahusika wanakamatwa.

“Kila anayekamatwa na madawa ya kulevya au na kitu chochote ambacho siyo halali, anafunguliwa mashtaka. Mimi naishi kwenye Jiji la Qingyuan, nimeshahuhudia Mtanzania mmoja, Wanigeria wawili na Waghana watatu wakikamatwa.
“Kote hakuna kupumua, hata huko Guangzhou, Beijing na kwingineko kunatisha kwa msako. Nasikia kwenye Mji wa Shanwei alikamatwa Mtanzania mwingine, akakutwa na ungaunga wa marumaru ambao alikuwa nao kama sampuli kwa ajili ya biashara zake, alikamatwa lakini aliachiwa baada ya kupimwa na kugundulika siyo madawa ya kulevya.”
Habari zaidi zinasema kuwa pamoja na sifa mbaya ya Watanzania nchini humo lakini imebainishwa kwamba Wanigeria ndiyo kundi hatari na wanawindwa zaidi kwa sababu raia wa nchi hiyo wameshachafuka sana.
Imebainishwa zaidi kuwa kwa vile siyo rahisi kumtofautisha Mnigeria na Waafrika wengine kwa haraka, ndiyo maana kila Mwafrika anapoonekana ni lazima ale msoto wa kukaguliwa ili kuhakikisha kama ana ‘mzigo’ au hana.
Risasi Jumamosi linamiliki picha zinazowaonesha baadhi ya Waafrika wakiwa chini ya ulinzi, wakitembezwa vifua wazi, kueleka vituo vya polisi kufunguliwa mashtaka ya uhalifu mbalimbali ikiwemo madawa ya kulevya.

KINACHOWAPONZA NI HIKI
Kwa mujibu wa taarifa kutoka China, taifa hilo limeshtukia kwamba pamoja na sheria kali za udhibiti wa madawa ya kulevya zilizopo na adhabu kali ikiwemo ile ya juu kabisa ya kunyongwa hadi kufa kwa mtu anayekutwa na hatia ya kujihusisha na biashara hiyo, polisi wameendelea kupigwa bao la kisigino.
Imeelezwa kwamba watu wanaosafiri na madawa ya kulevya tumboni, maarufu kama punda ndiyo wanaofanya madawa yazagae nchini humo.
“Punda ndiyo wanatuponza, Serikali ya China imeshtukia kuona kwamba madawa yapo sana mitaani, kwa hiyo kukomesha kabisa hilo, wanafanya msako hatari sana. Wakifika chumbani kwako utajuta, wanapekua kila upande wa chumba.
“Vilevile ikitokea mtu anawasili uwanja wa ndege akiwa dhaifu, anafuatiliwa sana. Asikwambie mtu, hakuna Mwafrika aliyepo China anayeishi kwa raha, iwe unauza au huuzi lazima uhenyeshwe,” alisema Dominick Rafiki anayeishi Guangzhou, China.

CHINA YASISITIZA KUENDELEA KUNYONGA
Ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International mwaka 2012, iliitaja China kama taifa kinara kwa kunyonga watu wenye makosa mbalimbali na kuitaja nchi hiyo kama katili zaidi duniani.
Amnesty International inapingana na adhabu ya kifo, kwa hiyo imekuwa ikitumia jitihada mbalimbali kuhakikisha linaishawishi China iachane na hukumu za kunyonga watu bila mafanikio.
Shirika hilo lilieleza kwamba China imeendelea kuweka msisitizo wa kunyonga watu, huku ikiwa na rekodi ya kunyonga maelfu ya watu kila mwaka.

BALOZI AKIRI HALI NI MBAYA
Balozi mpya wa Tanzania nchini China, Luteni Jenerali Mstaafu, Abdulrahman Shimbo amekiri kwamba hali ni mbaya kutokana na wimbi kubwa la Watanzania kukumbwa na kashfa ya madawa ya kulevya, huku wengine wakiwa wameshahukumiwa kunyongwa.
“Ni kweli hali ni mbaya, kuna vijana wetu wengi wanaipa sifa mbaya nchi yetu hapa. Kama inavyofahamika, mimi bado mgeni lakini nikipewa muda kidogo nitakuwa na ripoti kamili ya jinsi Watanzania wanavyohusishwa na hii biashara haramu ya madawa ya kulevya,” alisema Balozi Shimbo ambaye alikuwa Mnadhimu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)

Ijumaa, 30 Agosti 2013

"KAJALA NDIO KILA KITU KWANGU KWA SASA, YEYE NI ZAIDI YA MUME KWANGU"

KASUMBA ya wanawake wengi kuwaambia mashoga zao siri zao nzito inadaiwa kumfanya msanii maarufu wa filamu Bongo, Wema Sepetu kufunguka kuwa, bila kuwa karibu na Kajala Masanja itakuwa ni kama kuamua kutembea mtupu.

Wema alifikia hatua ya kutoa maneno hayo katikati ya wiki hii kwa kuposti picha kwenye mtandao wa Instagram ikimuonesha yeye, meneja wake Martin Kadinda na Kajala huku akisindikiza na ujumbe mzito uliosomeka:
“I always call my poch and I fell so naked without, I need her everywhere with me. I hope that’s how they out each other.”
Aliandika kimombo, alimaanisha nini?
Tafsiri ya maneno hayo ni kwamba, Wema anamchukulia Kajala kama pochi yake na bila yeye anajihisi yuko uchi kiasi kwamba anataka kila sehemu wawe wote.
Kajala amjibu
Baada ya Wema kutundika ujumbe huo, Kajala naye alijitutumua na kutupia maneno ya kumshukuru (Wema) huku akieleza kuwa, kama ni hivyo yeye hana la kusema.
“Nimeyapenda maneno hayo, kama ni hivyo mimi sina la kusema,” aliandika Kajala kwenye mtandao huo.
Kwa nini Wema aseme hivyo?
Yawezekana Wema alimaanisha vingine lakini wachambuzi wa mambo wamekuwa na maoni yao huku wengi wakieleza kuwa, inawezekana Wema anasema hivyo kutokana na ukweli kwamba Kalaja anajua siri zake nyingi.
“Unajua Wema amekuwa na marafiki wengi sana lakini inavyoonekana Kajala amemshiba sana na anajua siri zake nyingi. Wema anaposema bila Kajala itakuwa ni kama anatembea uchi anamaanisha kuwa, wakikorofishana kuna hatari ya kuanikana mambo yao nyeti.

“Watu wanazusha kuwa Wema anauza ‘unga’, mara anatembea na kigogo mmoja serikalini, ukweli wa haya anaujua Kajala na ndiyo maana amemshiba ili siri zake ziendelee kuwa sirini,” alidai mmoja wa marafiki wa karibu wa Kajala aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mariam wa Kinondoni alisema: “Hawa wana siri nzito, kila mmoja anajua mambo ya ndani ya mwenzake na ndiyo maana hakuna ambaye yuko tayari kumtosa mwenzake, watazinguana lakini watarudiana.”
Kajala anasemaje?
Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Kajala kuzungumzia maoni yake juu ya ujumbe huo wa Wema ambapo alisema, hana neno la kutia isipokuwa amefarijika tu kusikia anapendwa kiasi hicho.
“Kwa kweli hata kama wewe unaambiwa hivyo lazima utafurahi sana maana sikuwa najua kuwa napendwa na shosti wangu (Wema) ila hata mimi nampenda sana yaani siwezi kueleza, hayo manenomaneno ya watu hatuwezi kuyasikiliza,” alisema Kajala.
Msikie Wema
“Nilichokiandika nilikimaanisha, Kajala kwa sasa siyo rafiki yangu tena ni ndugu ambaye nampenda sana kutoka moyoni mwangu na nitampenda siku zote na ndiyo maana sijisikii kuwa mbali naye,” alisema Wema.
Watadumu?
Swali ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza ni kama ushosti wa wawili hao utadumu kwani mara kadhaa imekuwa ikidaiwa kuwa wametibuana na baadaye kuonekana wako pamoja, mazingira yanayoashiria kuwa huenda siku moja wakazinguana moja kwa moja.
Hayo yanakuja kufuatia historia ya Wema ambaye amekuwa hadumu na marafiki zake, mfano ukiwa kwa msanii Snura Mushi (staa wa Majanga) ambaye waliwahi kuwa marafiki kupitiliza lakini baadaye wakatosana

MAMBO YA SHILOLE HAYO NDANI YA FIESTER


Dance imekolea kwa shilole hapo ...mpaka mambo yote hadharani ......kitu cha black

Jumanne, 27 Agosti 2013

VIGOGO 111 WANAOJIHUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA WAMEANZA KUONJA JOTO YA JIWE....!!!




VIGOGO 111 wanaosadikiwa kujihusisha na biashara yharamu ya madawa ya kulevya nchini wameanza kuonja 'joto ya jiwe' kufuatia Jeshi la Polisi Tanzania Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kukamata mali zao, Uwazi lina mpango mzima.
Kwa mujibu wa vyanzo makini ndani ya jeshi hilo, pia vigogo wengi wanaojihusisha na biashara hiyo  walikamatwa na kiasi kikubwa cha ‘unga’ ndani ya kipindi cha miaka minne iliyopita.
Kuhusu mali ambazo ni magari, ilidaiwa kuwa kufuatia taarifa zilizowataja wauza unga, jeshi la polisi liliamua kushikilia magari hayo na kufanya uchunguzi wa uhalali wake.“Kuna watu walitajwa majina, wakafuatiliwa, magari yao yakakamatwa na kufanyiwa uchunguzi, lakini cha kushangaza baadhi yao  wameingia mitini na kutelekeza magari yao,” kilisema chanzo.
Chanzo kilisema baadhi ya magari hayo ni Mercedes Benz, Jeep, Toyota Spacio, Toyota Galsira, Toyota Mark II, Nissan Patrol 4x4 GL, Toyota Land Cruiser na Toyota Prado.   
Uwazi lilifanikiwa kunasa majina ya vigogo waliokamatwa wakiwa na unga  na kiasi walichokamatwa nacho.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika mahakama mbalimbali nchini na ndani ya jeshi la polisi umebaini kuwa, kesi za watuhumiwa hao zinaendelea kuunguruma kortini  japokuwa kasi yake si ya kuridhisha.Na Global publisher


VIGOGO 111 wanaosadikiwa kujihusisha na biashara yharamu ya madawa ya kulevya nchini wameanza kuonja 'joto ya jiwe' kufuatia Jeshi la Polisi Tanzania Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kukamata mali zao, Uwazi lina mpango mzima.
Kwa mujibu wa vyanzo makini ndani ya jeshi hilo, pia vigogo wengi wanaojihusisha na biashara hiyo  walikamatwa na kiasi kikubwa cha ‘unga’ ndani ya kipindi cha miaka minne iliyopita.
Kuhusu mali ambazo ni magari, ilidaiwa kuwa kufuatia taarifa zilizowataja wauza unga, jeshi la polisi liliamua kushikilia magari hayo na kufanya uchunguzi wa uhalali wake.“Kuna watu walitajwa majina, wakafuatiliwa, magari yao yakakamatwa na kufanyiwa uchunguzi, lakini cha kushangaza baadhi yao  wameingia mitini na kutelekeza magari yao,” kilisema chanzo.
Chanzo kilisema baadhi ya magari hayo ni Mercedes Benz, Jeep, Toyota Spacio, Toyota Galsira, Toyota Mark II, Nissan Patrol 4x4 GL, Toyota Land Cruiser na Toyota Prado.  
Uwazi lilifanikiwa kunasa majina ya vigogo waliokamatwa wakiwa na unga  na kiasi walichokamatwa nacho.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika mahakama mbalimbali nchini na ndani ya jeshi la polisi umebaini kuwa, kesi za watuhumiwa hao zinaendelea kuunguruma kortini  japokuwa kasi yake si ya kuridhisha.Na Global publisher


POLISI WABUNI MBINU MPYA
Vyanzo hivyo viliendelea kudai kwamba polisi wamebuni mbinu mpya ya kuwakamata vigogo wa madawa ya kulevya wakiamini itawapa mafanikio zaidi.
“Siku hizi si kama zamani, jeshi la polisi tumebuni mbinu mpya ya kuwakamata hawa jamaa (vigogo). Mbinu hii italeta mafanikio makubwa zaidi,” alisema mtoa habari wetu.

WAPAMBANAJI WA UNGA HATARINI
Taarifa zaidi zinadai kwamba usalama wa viongozi wanaopambana na wahusika wa unga nchini upo shakani kutokana na vitisho vinavyotolewa na mtandao huo duniani kote.
Inaaminika kuwa wengi wanaopambana au kupiga vita madawa ya kulevya, hususan viongozi na waandishi wa habari, hutendwa vibaya wakati mwingine kuuawa kabisa.

UWAZI LAMSAKA KAMANDA NZOWA
Kufuatia taarifa hizo za kiuchunguzi, katikati ya wiki iliyopita, mapaparazi wetu walimtafuta Kamanda wa Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa na kumuuliza kuhusu zoezi zima la kamatakamata ya wanamtandao hao.
Kamanda Nzowa alisema zoezi la kuwakamata wanaojihusisha na biashara hiyo linaendelea vizuri.
Alisema mpaka Mei, mwaka huu kikosi chake kimeshakamata kiasi kikubwa cha unga na kuongeza kuwa anaamini kasi ya biashara hiyo nchini imepungua sana.
Aliongeza kuwa askari wake wamejipanga vizuri na wana mafunzo maalum ya kuwatambua watu hao hatari.

VIGOGO HUWALISHA KIAPO KIBAYA  WANAOWABEBESHA
“Tumewakamata ‘mapapa’ (wauza unga wadogo) wengi sana na tunahakikisha kwamba ‘nyangumi’ (wauza unga vigogo)  nao hawachomoki.
“Mara nyingi vigogo wamekuwa wakiwalisha kiapo kibaya vijana wanaowabebesha unga kwamba  ikitokea wakakamatwa wasiwataje lakini nao tunawabana kitaalam mpaka wanawataja, kwa sasa bado tunaendelea kuwadaka,” alisema Kamanda Nzowa.
Kamanda huyo aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi lake dhidi ya wauza madawa ili kutokomeza kabisa biashara hiyo.

ULINZI VIWANJA VYA NDEGE NCHINI SASA NI MOTO
Katika maongezi yake, Afande Nzowa alisema ulinzi umeimarishwa katika viwanja vya ndege, bandarini, mipaka ya nchi na sehemu zote zinazohisiwa kuweza kupitishwa madawa hayo.

AANIKA MAJINA 111
Kamanda Nzowa alikwenda mbele zaidi kwa kuweka wazi takwimu ya ukamataji wa watuhumiwa hao kutoka mwaka 2009 hadi Mei, 2013.
Orodha chini inabainisha kiasi na aina ya madawa waliyokamatwa nayo katika mabano.
Steven  Gwaza, (heroin gramu 825.7), Rebecca Wairimu Mwangi (heroin gram 1,800), Khatibu Bakari Khatibu, Khalid Salim Maunga, (cocaine gramu 1,007.4), Dhoulkefly  Awadh, (cocaine gramu 893.58), Abdallah Pashua Kipevu (heroin gramu 31,000), Diaka Brama Kaba (heroin gramu 31,000), huyu alikamatwa akiwa na Ndjane Abubakar, Sylivia Kaaya Namirembe, Farid Kisuule, Robinson Dumba Teise na Ismail Mugabi.
Wengine ni Rashid Salim Mohamed, (cocaine gramu 1,374.32), Mini Thabo Hamza (cocaine gramu 1,595.74), Hamis Mohamed Mtou (cocaine gramu 850), Kwako Sarfo, Mnigeria (cocaine gramu 1,1951.80), Mustapha Musa (cocaine gramu 286), alikuwa na Aman Saidfadhil Daruweshi na Afshin  Jalal.
Kamanda Nzowa akaendelea kuwaanika, Jack Vuyo, (heroin gramu 42,000) huyu alikuwa na Anastazia Elizabeth Cloete. Simon Eugenio Fadu    (cocaine gramu 8,000), Assad  Aziz, (heroin gramu 50,000), alikuwa na Isamil Shebe Ismail, Rashid Salim na Majed Gholamghader.
Wengine kwenye orodha hiyo ni, Anna  Jamaniste Mboya, (cocaine gramu 1,140), Fredy William Chonde (heroin gramu 175,000),  Kambi Zuber, Abdul Ghan na Shahbaz Malik, Livinus Malik (Wapakistani) (cocaine gramu 804.7), Chukwudu  Denis Okechukwu, Paulo Ekechukwu na Hycenth Stan (Wanigeria) (cocaine gramu 81,000).
Aidha wapo, Shoaib S.O. Mohammed, Fedro Alfredo Chongo, (cocaine gramu 1,530), Kadiria  Said Kimaro (heroin gramu 1,365.91),  Abdallah Rajab Mwalimu (cocaine gramu 716.5), Mwiteka Godfrey Mwandemele (cocaine gramu 1,112),  Abbas Kondo Gede (cocaine gramu 1,112), Mwanaidi  Ramadhan Mfundo (cocaiane gramu 5,000), alikuwa na Sarah David Munuo,  Antony  Karanja, Benny Ngare,  Almasi Hamis Said, Yahya Haroun Ibrahim, Aisha Said Kungwi, Rajab Juma Mzome na John  William Mwakalasya.
Wengine ni Ally Mirzai Pirbakhshi (cocaine gramu 97,000) alikuwa na Aziz Juma Kizingiti, Said Mashaka Mrisho, Abdulahman  Mtumwa na Hamidu Kitwana Karimu.
Ramadhan Athuman (heroin gramu 3,000) alikuwa na Rashid Mohammed, Ally Mohammed Kichaa na Issa Abdulahman. Rashid  Ally Mtopea (heroin gramu 12,000) alikuwa na Idd Adam Mwaduga, Nurdin Adam. Maurine Amatus Lyumba, John  Adams Igwenma  wa (Mnaijeria) ( cocaine gramu 830.19).
Upendo Mohammed Cheusi, Abdallah Omar Salum (cannabis sativa gramu 1,000) alikuwa na Cosmos Chukwumezie, Ifeanyi  Malven Kalu Oko (Wanaijeria)  (heroin gramu 3,185.38), Allan Duller (cocaine gramu 3,882.92), Alberto Mendes kutoka Ghana, (gramu 1,277.10 za heroin)
Wengine ni Joseph Chukwumeka Nwabunwanne Minigeria, (gramu 1,245.96 za heroin) Kwaku Safo Brobbey Mghana (gramu 13,781.78 za heroin), Princewill Ejike Mnigeria (gramu 981.12 za heroin),Mary  Mvula Mzambia (gramu 391.51 za cocaine), Waziri Shaban Mizongi, (gramu 2,013 za heroin) akiwa na Santos Joseph Mpondela, Kelvin Kelven Mwazeni.
Wengine ni Emmanuela Adom, Mghana (gramu 9,838.1 za cocaine), Asha Omary Ramadhan, (gramu 1.56), Mariam Mohammed Said, (gramu 9,857.54 za bangi) akiwa na Abdullatif A. Fundikira
Aliendelea kuwataja Marceline Koivogui, Mghana (gramu 1,073.82 za heroin),  Edwin Cheleh Swen Mliberia (gramu 1,509.35 za heroin),  akiwa na Benjamin Obioma Onuorah  wa Nigeria, Sofia Seif Kingazi, (gramu 3,379.54 za cocaine), Josephine Mumbi Waithera Mkenya (gramu 3,249.82 za cocaine), Iddi Juma Mfaume,( gramu 563.25 za heroine), Amina Kassim Ramadhani,( gramu 1,980.11 za heroine) na Vivian Edigin Mnigeria ( gramu 797.56 za cocaine), Hadija Tambwe,( gramu 33,507.04 Za cannabis),  Sasha Farhan  na Mnyeke Sativa, na Mychel Andriand Takahindangeng Muindonesia,( gramu 3,932.44 za cocaine).
Wengine ni Kristina Biskavevskaja Mluthenia (gramu 4,000 za cocaine), Stephen Basil Ojiofor Mnigeri (gramu 1,173 za cocaine), Judith Marko Kusekwa, ( gramu 1,793 za heroin), Khamis Said Bakari,( gramu 1,793 za heroin).
Kundi la mwisho ni Tabia Omary au Neema Omary (gramu 994.97 za  heroin), Masesa au Habiba Andrew Joseph, ( gramu 1,037.9 za heroin).
Hivi karibuni Agness Gerald ‘Masogange’ na mwenzake walikamatwa Afrika Kusini wakiwa na kilo 150 za dawa za kulevya.

HILI NDO JESHI ALLILOLITAMBULISHA WEMA SEPETU KWENYE SHOW YAKE

Wema sepetu atambulisha jeshi lake rasmi usikuWa kuamkia Leo... Ilikuwa ni zaidi ya burudani









ASALI AKIMTAMBURISHA MZURI WAKE....































Mwananchi wa kawaida akiteremsha ratiba nzima ya show....
Mnyama akifanya yake....