Alhamisi, 26 Septemba 2013

UNAMKUMBUKA YULE MSANII FUSKA MANAIKI SANGA?? IRENE UWOYA NAYE KAWEKWA KATIKA LISTI YAKE..!! TAZAMA PICHA ZAO HAPA..!!


 Wasanii Manaiki Sanga na Irene Uwoya wakiwa kwenye picha za mahaba huku Uwoya akigida bieeeee hadi kuche.

Na Mwandishi Wetu
Mtandao hatari wa habari wa Xdeejayz kwa mara nyingine umekuwa wa kwanza kunasa picha za wasanii mastaa toka kiwanda cha bongo movie Manaiki Sanga na Irine Uwoya zikiwaonesha wakiwa kwenye mahaba mazito huku Irine akiwa ho kwa kiraji “pombe”.

 Habari makini toka chanzo chetu makini ambacho ni rafiki wa karibu na Irine Uwoya kilisema Irine na Manaiki kwa sasa wako kwenye mahusiano ya karibu kiasi cha kuzua minong’ono kwa kudhani huenda wanamahusiano ya upande wa pili.

Hata hivyo chanzo hicho kiliendelea kusema kwa picha hizo zinadaiwa kupigwa katika viunga vya Club Maisha ambako walienda kula bata usiku kucha na hapo inaonekana ni asubuhi.

Aidha xdeejayz ilifanya juhudi za kuwatafuta wasanii hao ili kuweka bayana kuhusu picha zao hizo za mahaba na Uwoya ndiye aliyeanza kuvutiwa waya lakini hata hivyo simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa na alivyopigiwa Manaiki Sanga na baada ya mwandishi wetu kujitambulisha na chombo cha habari anachotoka hali ilikuwa tofauti kidogo kwani msanii huyo alianza kumporomoshea matusi makubwa mwandishi wetu huku akiituhumu blog hii kuongoza kumchafua kwa kuanika mambo yake ya siri hadharani.
 Mtandao hatari wa habari wa Xdeejayz kwa mara nyingine umekuwa wa kwanza kunasa picha za wasanii mastaa toka kiwanda cha bongo movie Manaiki Sanga na Irine Uwoya zikiwaonesha wakiwa kwenye mahaba mazito huku Irine akiwa ho kwa kiraji “pombe”.
Habari makini toka chanzo chetu makini ambacho ni rafiki wa karibu na Irine Uwoya kilisema Irine na Manaiki kwa sasa wako kwenye mahusiano ya karibu kiasi cha kuzua minong’ono kwa kudhani huenda wanamahusiano ya upande wa pili.
Hata hivyo chanzo hicho kiliendelea kusema kwa picha hizo zinadaiwa kupigwa katika viunga vya Club Maisha ambako walienda kula bata usiku kucha na hapo inaonekana ni asubuhi.
Aidha xdeejayz ilifanya juhudi za kuwatafuta wasanii hao ili kuweka bayana kuhusu picha zao hizo za mahaba na Uwoya ndiye aliyeanza kuvutiwa waya lakini hata hivyo simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa na alivyopigiwa Manaiki Sanga na baada ya mwandishi wetu kujitambulisha na chombo cha habari anachotoka hali ilikuwa tofauti kidogo kwani msanii huyo alianza kumporomoshea matusi makubwa mwandishi wetu huku akiituhumu blog hii kuongoza kumchafua kwa kuanika mambo yake ya siri hadharani.


Jumatano, 25 Septemba 2013

WANAFUNZI 300 ELIMU YA JUU KUKOSA MIKOPO

Zaidi ya wanafunzi 300 wa elimu ya juu wa vyuo mbalimbali watakosa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kutokana na kushindwa kujaza fomu za kuomba mikopo katika kipindi kilichowekwa. 
Watakaokosa mikopo hiyo kwa mwaka wa masomo wa 2013/2014 ni kuanzia mwaka wa pili na kuendelea, ambao hawakujaza fomu za kuonyesha taarifa zao mpya kwa bodi. 
Wanafunzi hao walitakiwa kuwasilisha maombi ya kupewa mikopo kati ya Mei hadi Julai 30, mwaka huu.
Mkugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HELSB, Cosmas Mwaisobwa, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi kuhusu utendaji wa kazi wa bodi hiyo. 
Mwaisobwa alisema kwa kuwa wanafunzi hao hawakujaza fomu za kuomba mikopo, mwaka huu hawatapata fursa hiyo na kwamba kwa mujibu wa utaratibu wao, kila mwaka lazima mwanafunzi aombe. 
Alisema wanafunzi watakaokosa fursa hiyo ya mikopo wameanza masomo yao katika vyuo mbalimbali nchini na kwamba  HESLB haijui sababu zilizowafanya wasiombe. 
Kuhusu ufanisi katika utoaji wa mikopo, Mwaisobwa alisema idadi ya wanafunzi wanaoomba mikopo imeongezeka kutoka 42,729 mwaka 2005/2006 hadi kufikia wanafunzi 97,348 mwaka 2012/2013. 
Aidha, Mwaisobwa alisema bajeti ya kuwakopesha wanafunzi imeongezeka kutoka Sh. bilioni 56.1 mwaka 2005/2006 hadi kufikia Sh. bilioni 306 mwaka 20012/2013. 
Alisema mwaka huu serikali imeitengea bodi hiyo Sh. bilioni 325 kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi wapya, 31,647 na 62,376 wanaondelea na masomo yao katika vyuo mbalimbali. 
Wakati wanafunzi hao wakikosa fursa ya mikopo, mapema mwezi huu, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, aliitaka bodi hiyo kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi na weledi mkubwa kwa mwaka huu wa masomo ili kuepusha migogoro ya wanafunzi kuhusu mikopo.
CHANZO: NIPASHE

MAALUM KWA WANAWAKE WANAO TAKA KUOLEWA

 
 Hata kama utapingana na mimi, lakini ukweli utabaki pale pale; Kila jinsia inahitaji sana kuungana na jinsia nyingine katika tendo muhimu na la kihistoria katika maisha liitwalo ndoa! Yes, huu ni ukweli ambao upo

wazi na utaendelea kusimama kama ulivyo.
Jinsia zote zina umuhimu na jambo hili muhimu, lakini kuna tofauti kidogo, kwamba mwanamke
anasubiri kufuatwa na mwanaume, wakati mwanaume anaamua kumfuata mwanamke anayemtaka na kwa wakati wake. Kuna kitu nataka kuweka sawa hapa, kwamba wanaume ndiyo huwa wa kwanza kupenda kabla ya mwanamke, ingawa mwanamke anaweza kuwa wa kwanza kupenda lakini akashindwa kufikisha hisia zake kwa mwanaume husika.
Wanawake wa ‘mjini’ huwa hawakubaliani na hili, kutokana na huu utandawazi unaohubiriwa siku hizi ikiwa ni pamoja na kampeni za usawa zinazotetewa na Wanaharakati Wanawake. Akina dada nao huchangamkia kueleza hisia zao kwa wanaume. Nadhani si jambo baya, ingawa linaweza kupokelewa kwa hisia tofauti na kila mwanaume.
Tuyaache hayo, hoja kubwa ya msingi hapa ni jinsi gani mwanamke anaweza kuolewa haraka na mpenzi wake. Ikumbukwe kwamba, hapa nazungumza na wanawake ambao tayari wapo katika uhusiano, lakini wenzi wao hawana habari kabisa na mambo ya ndoa.
Katika matoleo yaliyopita, niliwahi kuzungumza kuhusu namna gani mwanamke anaweza kuwashawishi wanaume wakataka kuingia katika uhusiano naye. Leo nazungumzia juu ya wewe ambaye upo katika uhusiano ambao haueleweki, lakini ndoa unaitaka. Unajua cha kufanya? Fuatana nami.
EPUKA MAKUNDI HATARI
Mwanaume anapenda kuwa na mke mwenye staha, ambaye hana tabia za hovyo. Kuwa na makundi ya ‘mashangingi’ ni alama ya kwanza kabisa kuwa unapenda au tayari una tabia za kishangingi. Wanaume wengi hawapendi kabisa wanawake wenye tabia za hovyo, wenye kampani ambazo si nzuri.
Lakini yawezekana, jamaa alishakuambia juu ya kilio chake hiki, lakini wewe umekuwa kama umeweka pamba masikioni mwako, hili ni tatizo. Linda heshima yako, kaa mbali na makundi hatari, ili umfanye jamaa akuone wewe ni mwanamke thabiti ambaye huigi, hushabikii na wala huna tabia mbaya. Utaonesha hili kwa kukaa mbali na makundi ya wanawake hatari! Umenipata?
ZINGATIA MAVAZI YAKO
Kila mtu anamjua mtu wake alivyo, mwanamke hata wewe unamjua mpenzi wako alivyo. Sina shaka unafahamu anapenda nini na nini anachukia. Unajua kabisa, nina uhakika na hilo. Lakini pamoja na kwamba jamaa anaweza kuwa na vitu ambavyo vinamvutia zaidi, hata wewe kama mtoto wa kike, una mapendekezo yako au vitu ambavyo unapenda zaidi kuvifanya!
Huzuiwi, lakini swali la msingi, mwenzi wako anapenda? Kama wewe unapenda sana skin jeans na top inayoacha kitovu nje, yeye hapendi kwa sababu ana nia ya kukufanya mke hapo baadaye. Sasa utakuwa mke gani ambaye hata Salim anaona sehemu zako za faragha hadharani?
Ukiachana na chaguo la mwenzi wako, lakini lazima wewe mwenyewe kama mwanamke wa mtu, ujitambue! Jisitiri vyema. Kwani kuna urembo gani wa kuvaa nguo inayoonesha mwili wako ulivyo? Kuna burudani gani kuacha nyeti zako wazi? Unataka nani akuone ulivyo? Mke hana sifa hiyo dada yangu, sasa ili uweze kuwa na sifa hii muhimu, lazima uzingatie sana mavazi yako.

JIPE MOYO
Hili nilishawahi kulizungumza sana katika mada zilizopita, baadhi ya wanawake wamekuwa wakikatishwa tamaa na rafiki zao au watu wengine wanaowazunguka, eti hawana hadhi ya kuolewa au watahangaika sana lakini hawatapata mume, kisa eti HAVUTII!
Mwingine anajinyima mwenyewe nafasi akisema; “Mimi nina balaa, sina bahati ya kuolewa, ndiyo maana wadogo zangu wote wameolewa nimebaki mimi.”
Huu ni uvivu wa kuwaza. Lakini dada yangu, habari iliyo njema kwako ni kwamba, ndoa unaitengeneza wewe mwenyewe.
Unaitengeneza kwa misingi ya kwanza, kujipa moyo mwenyewe kwamba wewe ni mzuri na una sifa na haki za kuolewa kama wanawake wengine. Jipe moyo mwenyewe, huna nuksi wala balaa, wewe ni mzuri na una sifa za kuwa mke hapo baadaye.

Iko hivi, ukianza kujishusha mwenyewe, ni dhahiri kwamba hata mavazi yako hayatakuwa mazuri, uso wako hautakuwa na tabasamu na wala hutakuwa na matumani moyoni, hapo sasa ni mwanzo wa kuzorota afya yako. Utapata mchumba kweli? Utasubiri sana kwa mtindo huo.
ACHA PAPARA
Haizuiwi kuuliza kuhusu mustakabali wa uchumba wenu, lakini ni vizuri basi kuwa na kiasi. Kuuliza kila wakati au kuwa mtu wa kulaumu, hakutakusaidia kumfanya jamaa achukue maamuzi ya haraka ya kukuoa na badala yake yanaweza kumpa picha tofauti.
Ni rahisi kuwaza kwamba, unachohitaji kwake ni ndoa na baada ya hapo hutakuwa na staha tena. Kuwa mjanja, achana na papara. Usilogwe ukamfanyia jambo zuri mpenzi wako, halafu ndiyo umuulize; “Sasa honey, mbona hata huzungumzii ndoa yetu? Hivi utanioa kweli? Eeeh baby? Niambie basi mpenzi wangu.

Jumanne, 24 Septemba 2013

PICHA: I AL SHABABY WAKIWA NDANI YA WESTLAND

Suspected AlShabaab fighters inside #Westgate. Look how comfortably they are walking around as if they're shopping

Jumatatu, 2 Septemba 2013

HAYA NDO YANAYOWAKUTA WATANZANIA WALIOKAMATWA NA MADAWA HUKO CHINA

Stori: Na Mwandishi Wetu
Taifa la China halina mzaha mbele ya biashara haramu ya madawa ya kulevya na kwa kutambua kwamba wanaohusika zaidi ni Waafrika, sasa hivi kila mja mwenye ngozi nyeusi aliyepo nchini humo, anapewa msoto wa nguvu.

Wabongo wanaoishi China, kwa sasa wanahenyeshwa isivyo kawaida katika msako uliopewa jina
na Watanzania kwamba ni Oparesheni Safisha Wauza Unga.
Katika hoteli wanazofikia, vijiwe vyao, barabarani na kadhalika, kote huko wanapewa msoto wa guvu kwa kile kinachoelezwa kuwa Wachina hawana imani tena na Watanzania na Waafrika kwa jumla ama wanaoishi nchini humo au hata wale wanaoingia na kutoka.

“Wazungu wa unga (wafanyabiashara wa madawa ya kulevya) wanatuharibia starehe hapa China, hatuishi kwa amani tena. Mtu unaweza kukaguliwa siku nzima kisa eti wanawatafuta wanaouza unga,” alisema Artides Kimota ambaye ni Mtanzania anayeishi China kwa sasa.

Aliongeza: “Unajua sasa hivi China imekuwa na uingizwaji mkubwa wa madawa ya kulevya. Kwa Serikali ya China hii ni kashfa nzito. Kwa vile wanajua Waafrika ndiyo sababu kuu, sasa hivi kila Mwafrika anapewa msukosuko.

“Kwa kweli ukiwa Mwafrika hapa China ni mateso makubwa sana kwa sasa. Kuna agizo la serikali ambalo limelitaka jeshi la polisi hapa China kuhakikisha madawa ya kulevya yanatokomezwa na wahusika wanakamatwa.

“Kila anayekamatwa na madawa ya kulevya au na kitu chochote ambacho siyo halali, anafunguliwa mashtaka. Mimi naishi kwenye Jiji la Qingyuan, nimeshahuhudia Mtanzania mmoja, Wanigeria wawili na Waghana watatu wakikamatwa.
“Kote hakuna kupumua, hata huko Guangzhou, Beijing na kwingineko kunatisha kwa msako. Nasikia kwenye Mji wa Shanwei alikamatwa Mtanzania mwingine, akakutwa na ungaunga wa marumaru ambao alikuwa nao kama sampuli kwa ajili ya biashara zake, alikamatwa lakini aliachiwa baada ya kupimwa na kugundulika siyo madawa ya kulevya.”
Habari zaidi zinasema kuwa pamoja na sifa mbaya ya Watanzania nchini humo lakini imebainishwa kwamba Wanigeria ndiyo kundi hatari na wanawindwa zaidi kwa sababu raia wa nchi hiyo wameshachafuka sana.
Imebainishwa zaidi kuwa kwa vile siyo rahisi kumtofautisha Mnigeria na Waafrika wengine kwa haraka, ndiyo maana kila Mwafrika anapoonekana ni lazima ale msoto wa kukaguliwa ili kuhakikisha kama ana ‘mzigo’ au hana.
Risasi Jumamosi linamiliki picha zinazowaonesha baadhi ya Waafrika wakiwa chini ya ulinzi, wakitembezwa vifua wazi, kueleka vituo vya polisi kufunguliwa mashtaka ya uhalifu mbalimbali ikiwemo madawa ya kulevya.

KINACHOWAPONZA NI HIKI
Kwa mujibu wa taarifa kutoka China, taifa hilo limeshtukia kwamba pamoja na sheria kali za udhibiti wa madawa ya kulevya zilizopo na adhabu kali ikiwemo ile ya juu kabisa ya kunyongwa hadi kufa kwa mtu anayekutwa na hatia ya kujihusisha na biashara hiyo, polisi wameendelea kupigwa bao la kisigino.
Imeelezwa kwamba watu wanaosafiri na madawa ya kulevya tumboni, maarufu kama punda ndiyo wanaofanya madawa yazagae nchini humo.
“Punda ndiyo wanatuponza, Serikali ya China imeshtukia kuona kwamba madawa yapo sana mitaani, kwa hiyo kukomesha kabisa hilo, wanafanya msako hatari sana. Wakifika chumbani kwako utajuta, wanapekua kila upande wa chumba.
“Vilevile ikitokea mtu anawasili uwanja wa ndege akiwa dhaifu, anafuatiliwa sana. Asikwambie mtu, hakuna Mwafrika aliyepo China anayeishi kwa raha, iwe unauza au huuzi lazima uhenyeshwe,” alisema Dominick Rafiki anayeishi Guangzhou, China.

CHINA YASISITIZA KUENDELEA KUNYONGA
Ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International mwaka 2012, iliitaja China kama taifa kinara kwa kunyonga watu wenye makosa mbalimbali na kuitaja nchi hiyo kama katili zaidi duniani.
Amnesty International inapingana na adhabu ya kifo, kwa hiyo imekuwa ikitumia jitihada mbalimbali kuhakikisha linaishawishi China iachane na hukumu za kunyonga watu bila mafanikio.
Shirika hilo lilieleza kwamba China imeendelea kuweka msisitizo wa kunyonga watu, huku ikiwa na rekodi ya kunyonga maelfu ya watu kila mwaka.

BALOZI AKIRI HALI NI MBAYA
Balozi mpya wa Tanzania nchini China, Luteni Jenerali Mstaafu, Abdulrahman Shimbo amekiri kwamba hali ni mbaya kutokana na wimbi kubwa la Watanzania kukumbwa na kashfa ya madawa ya kulevya, huku wengine wakiwa wameshahukumiwa kunyongwa.
“Ni kweli hali ni mbaya, kuna vijana wetu wengi wanaipa sifa mbaya nchi yetu hapa. Kama inavyofahamika, mimi bado mgeni lakini nikipewa muda kidogo nitakuwa na ripoti kamili ya jinsi Watanzania wanavyohusishwa na hii biashara haramu ya madawa ya kulevya,” alisema Balozi Shimbo ambaye alikuwa Mnadhimu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)