Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MATUKIO. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MATUKIO. Onyesha machapisho yote
Jumanne, 24 Septemba 2013
PICHA: I AL SHABABY WAKIWA NDANI YA WESTLAND
Suspected AlShabaab fighters inside #Westgate. Look how comfortably they are walking around as if they're shopping
Jumanne, 27 Agosti 2013
DAH HAYA MAENDELEO NOMA .. WENZETU WAMEWEKA VITUO VYA KUFANYIA NGONO KWENYE BARABARA
“Jiji limehalalisha na kufungua vyumba 9 ambavyo vitatumiwa na machangudoa na wateja wao kihalali na kwa usalama zaidi”
Vibanda(pichani kulia) tisa vya ngono vilivyojificha ndani ya uzio mkubwa vimeandaliwa kwaajili ya wauza miili ‘malaya’ na wateja wao kuanzia leo na kuendelea.
Kuna saini ndogo inayoonesha muda wa kazi, mwamvuli mwekundu kutambulisha eneo hilo kama eneo la shughuli hiyo ambalo zamani lilikuwa ni eneo la viwanda magharibi mwa jiji hilo.

Kuna eneo ambalo mteja anaweza kuchagua mwanamke anayemfaa, pamoja na makubaliano ya bei kabla ya kuelekea kwenye kibanda, ambacho ni cha mbao kinacho fanana na eneo la kuegesha gari.
Kila kiboksi kina alamu ili kuwalinda Malaya hao.
Michael Herzig, mkurugenzi katika huduma ya jamii ya wafanyakazi wa ngono jijini alisema “Umalaya ni biashara”
“Hatuwezi kuzuia, hivyo tunataka kudhibiti ili kuwasaidia wafanyakazi wa ngono na jamii, sababu bila kufanya hivyo uhalifu unaongezeka na wahuni wanazidi kuwa wengi”

Alisema “ hapa wanabakia humuhumu ndani na kuhudumia wateja wao haraka”
Eneo hilo la drive-in ya ngono limehalalishwa na wakazi wa Zurich katika sharia ya mwezi machi, 2012baada ya kupigiwa kura kwa asilimia 52.6 kukubaliana nalo.
Eneo hilo pia lina makubaliano mazuri tu yanayohusisha vyama vyote vya siasa nchini humo, likiwa na wanachama wengi wa chama cha Swiss People's Party (SVP) wanaopinga mpango huo.
"haitofanikiwa, labda kwasababu wateja hawatokuja au eneo hilo halitotumiwa na machangudoa” alisema Sven Oliver Dogwiler, mwanasiasa wa eneo hilo ambae ni mwanachama wa SVP
Jumatano, 21 Agosti 2013
ANGALIA PICHA ZA AJALI YA MSAFARA WA MWENGE PANDE ZA DODOMA
Ajali
hiyo iliyotokea jana majira ya 2;24 asubuhi katika mtelemko wa mlima fufu
wilayani Chamwino na kusababisha watu 5 kujeruhiwa na kukimbizwa katika
hospital ya mkoa wa dodoma.
Watu
hao ambao majina yao Bado hayajatambulika walipata majeraha katika maeneo mbali
mbali ya miili yao ikiwemo kichwani, kifuani, mguuni na mikononi.
Kaimu
Kamanda wa polisi Suzan Kaganda aliyefika na kujione hali ilivyokuwa katika
eneo hilo alisema chanzo cha ajali hiyo ni Matuta yaliwekwa kwenye Barabara
hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami toka fufu hadi Dodoma bila kuwa na alama
yoyote.
Jumanne, 20 Agosti 2013
ISHU YA PONDA KAMA MOVIE VILE

Mkurungenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), amemfutia mashtaka ya uchochezi Katibu wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, yaliyokuwa yanamkabili.
Jana saa 2:00 asubuhi viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu Hellen Riwa, upande wa Jamhuri uliwasilisha hati ya kusudio la kutokuendea na mashitaka kutoka kwa DPP.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka, aliwasilisha hati hiyo akidai kuwa DPP ameona hana nia ya kuendelea kumshtaki Sheikh Ponda na ameomba mahakama kumfutia mashtaka hayo.
MAJANGA: VAZI LA NUSU UCHI LAZUA KASHESHE KANISANI.. PADRI ASITISHA IBADA
KIVAZI cha ndugu wa maharusi, kimesababisha patashika katika Kanisa
Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Peter, baada ya Paroko Msaidizi wa Kanisa
hilo, Padri Paulo Haule, kusitisha ibada mpaka mhusika atoke akavae
vizuri.
“Ninatoa dakika 10 kwa aliyeingia na mavazi ambayo hayatakiwi kanisani humu kutoka mara moja akavae vizuri, la sivyo ndoa yao haitafungwa,” alisema Padri Haule wa Kanisa hilo lililoko Oysterbay, Dar es Salaam.
Awali vurugu hizo zilizotokea Jumamosi iliyopita, zilianzia nje, wakati Katekista wa Parokia hiyo, Yohane Maboko, alipotangazia wanandoa na ndugu zao waliokuwa mabega wazi au kuvaa nguo fupi, kutafuta nguo za kujifunika au wasiingie kabisa kanisani.
Maharusi walikubali kutekeleza ombi hilo, wakavishwa vitambaa mabegani vya rangi tofauti na gauni jeupe la harusi, wakaruhusiwa kuingia kanisani, tayari kufunga pingu zao za maisha.
Hata hivyo, mmoja wa ndugu wa maharusi hao ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alipotaka kulazimisha kuingia na kivazi chake cha mabega wazi, alizuiwa na Katekista Maboko. Katekista huyo alimfuata mwanamke huyo ili kumrudisha akavae vizuri, lakini aliibua zogo na kulazimisha kuingia na vazi hilo.
Zogo hilo lilipoendelea, wanandugu waliingilia kati, wakitetea vazi hilo ambapo mmoja wa wanandugu, alimvua miwani Katekista Maboko na kuipiga chini ikavunjika huku yeye na wenzake wakimtolea maneno makali ya kumtaka asimzuie ndugu yao kuingia kanisani.
Wakati ndugu hao wakimdhibiti Katekista Maboko, mwanamke huyo alitumia mwanya huo na kupenya hadi ndani ya Kanisa, ambamo Padri Haule, alikuwa akijiandaa kuanza ibada.
Baada ya Padri Haule kupata taarifa, alitangaza kuwa ndoa ya maharusi wa msichana huyo, haitafungwa hadi awe ametoka.
Licha ya Paroko kutangaza hivyo, bado ukaidi uliendelea jambo lililomfanya Katekista Maboko kumfuata tena dada huyo na kumwamuru atoke nje, ambapo aliendelea kupinga na baadaye akatekeleza amri hiyo ya Paroko.
Baada ya hapo shughuli za kufungisha ndoa ziliendelea kwa amani na utulivu hadi mwisho maharusi wakatoka kwenda kuendelea na mambo mengine.
Akizungumza na mwandishi wetu, Katekista Maboko alisema waumini hao walikiuka maadili ambayo Kanisa lina wajibu wa kulinda na kuyasimamia ili waumini wake wayafuate.
Alisema miwani yake iliyovunjwa ilikuwa na thamani ya Sh 90,000 na baada ya ibada hiyo, aliyetenda kosa hilo alimwendea na kumwomba radhi na kulipa Sh 50,000 na kuahidi kumalizia kiasi kilichobaki wakati wowote.
Maboko alisema uvaaji wa mavazi yasiyotakiwa kanisani hapo, umekuwa ukipigiwa kelele mara kwa mara, na hata katika mafundisho ya ndoa huambiwa lakini ukaidi unaendelea.
“Maharusi wakati wa mafundisho ya ndoa tunawaambia kuhusu mavazi yao na hata ya ndugu zao watakaowasindikiza kanisani, kuwa wavae kistaarabu lakini hawasikii,” alisema Katekista Maboko.
Makanisa mengi siku hizi yamekuwa yakipiga marufuku uvaaji wa nguo fupi na zinazoacha mabega wazi kwa wasichana na wanawake, wakati wa ibada za kawaida na za ndoa.

Jumatatu, 19 Agosti 2013
MAJAMBAZI WAVAMIA NA KUIBA KITUO CHA MAFUTA BUGURUNI
MAJAMBAZI jana yalifanya onesho la aina yake jijini Dar es Salaam, baada ya kupora mamilioni ya shilingi katika kituo cha mafuta cha Lake Oil, Buguruni Malapa na kumwaga fedha hizo kwa wananchi maeneo ya Tazara ili kuhadaa polisi.
Wakiwa katika pikipiki aina ya Toyo na fuko la fedha, majambazi hao baada ya kupora fedha hizo, walifanikiwa kupita katika foleni ya magari mpaka katika taa za Tazara.
Walipofika katika eneo hilo, ghafla polisi wenye silaha wakiwa katika pikipiki zaidi 10, walivamia na kusababisha majambazi hao kurusha sehemu ya fedha walizo pora hewani.
Shuhuda mmoja wa tukio hilo, anayeuza bidhaa mbalimbali akiwa amebeba mkononi katika eneo la Tazara, alieleza gazeti hili kuwa walijikuta wakikimbilia fedha hizo, kitendo kilichosababisha polisi kushindwa kutambua majambazi hao.
Kwa mujibu wa shuhuda huyo, wakati wananchi wakigombea fedha hizo, huku polisi wakihangaika kutaka kukamata watuhumiwa, majambazi hao walirukia gari aina ya Suzuki Pick Up.
Shuhuda huyo alidai majambazi hao walimwamuru dereva kuondoka, lakini dereva huyo alikumbwa na bumbuwazi, asijue la kufanya. Kutokana na kushindwa kuondoka, papo hapo walimjeruhi kwa risasi.
Muuza CD
Mtu mwingine ambaye alikuwa abiria katika gari hiyo, alipoona wamevamiwa, aliruka na kuanza kutimua mbio kwenda upande wa soko la Vetenari.
Hali hiyo ilisababisha polisi waliokuwa katika eneo hilo wakiwa na pikipiki, kuanza kumfukuza.
Gazeti hili lilishuhudia zaidi ya pikipiki nne za polisi, waliokuwa wakipiga risasi za moto hewani, wakimkimbiza abiria huyo, ambaye baadae alikutwa katika soko la Vetenari, karibu na ukuta wa TBC na aligundulika ni muuzaji wa CD za reja reja.
Baada ya muda mfupi, kundi la Polisi ambalo liliwasili katika eneo la tukio, lilifanikiwa kuwadhibiti majambazi hao, ambao awali walidaiwa kuwa watatu huku mmoja wao akiwa na silaha.
Polisi hao pia walionekana kuchukua fuko hilo la fedha na kuliingiza katika moja ya magari sita, yaliyokuwa na polisi hao. Aidha, watuhumiwa hao walipandishwa katika gari tofauti na lililobeba fedha hizo, huku wakivuja damu.
Gari hilo lilizungukwa na askari wa doria maalumu ya kudhibiti ujambazi jijini Dar es Salaam. Mbali na magari hayo, pia pikipiki za Polisi zilikuwa nyingi, jambo ambalo liliwatia moyo wananchi waliofika katika eneo hilo, kuwashuhudia majambazi hao na wengine walisikika wakisema ‘Polisi leo (jana) wamefanya kazi yao ipasavyo’.
Hata hivyo, wananchi hao walitaka wahalifu hao wasulubiwe papo hapo.
Akizungumza na gazeti hili, askari aliyekuwepo katika eneo hilo huku akikataa kutaja jina lake, alisema wamekamata majambazi wawili, ambao walipora fedha katika eneo la Buguruni Malapa na mmoja amekimbia.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema ofisi yake inakamilisha upelelezi, na leo taarifa kamili itatolewa kupitia Kanda Maalumu ya Kipolisi.
Ijumaa, 16 Agosti 2013
LADIES:JE WAJUA WANAUME WANAWEZA KUWEKWA KIGANJANI BILA WAGANGA?
Mbinu chache za kuwaweka waume zenu kiganjani.
Mpe mumeo anachohitaji :
Wanawake wengi wanashindwa kujua wao wanatofautiana na wanaume kwa
hisia na hata mawazo ya mapenzi. Wanaume wana mambo wanayoyapenda kutoka
kwa wake zao hasa katika masuala ya mapenzi. Kwanza wanawake wajue
wanaume wengi wana hisia za haraka za kufanya mapenzi kuliko wanawake.
HUYU NDO MTOTO NA CHURA WALIOZALIWA PAMOJA HUKO MBEYA
| Mtoto aliyezaliwa pamoja na kiumbe cha ajabu kinachofanana na chura |
| Mtoto akiwa na afya tele |
| Hiki ndicho kiumbe kilchotoka tumboni pamoja na mtoto mchanga kwa mama Matrida picha hii mara baada ya kutenganishwa na mtoto huyo |
![]() |
| Hapa ndipo kwa mkunga Agripina Sikanyika Matrida alipojifungulia watoto hao |
Alhamisi, 15 Agosti 2013
SHEKHE PONDA HATIMAYE APELEKWA SEGEREA
Hatimaye Sheikh Ponda Issa Ponda leo majira ya saa nn Asubuhi amepelekwa katika Gereza la Segerea.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyekuwepo
eneo la tukio ameipasha munirablog kwamba ilipofika majira ya saa nne
Asubuhi walikuja Maaskari na kumchukuwa Sheikh Ponda na kumpeleka
Gerezani Segerea.
,"Aah wamekuja Maaskari wengi
wakatufukuza fukuza wakaingia wodini wakaongea na Daktari
wake,wakaandika andika kisha wakamchukuwa na majeraha yake,wala
usisumbuke kuja kumuona,hapa hayupo yupo Segerea",alisema mpashaji wa
habari hizi.
Jumatano, 14 Agosti 2013
YALIYOJIRI MOSHI

MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Marangu
inayomilikiwa na kanisa Katoliki jimbo la Moshi, (jina limehifadhiwa)
alitekwa na kukufungiwa kwenye hoteli moja ya kitalii mjini hapa na
kufanyiwa vitendo vya ngono kwa muda wa siku nne mfululizo.
Jumatatu, 12 Agosti 2013
KAGAME AMJIBU KIKWETE
Serikali ya Rwanda imetoa tamko
linaloonyesha kutoielewa kauli ya Rais Jakaya Kikwete, iliyoamuru
wahamiaji haramu kuondoka nchini, hali inayoonekana kukwepesha hoja.
PICHA ZA SHEKHE PONDA AKIWA HOSPITALI YA MUHIMBILI
Sheik Ponda alipigwa risasi jana baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara Morogoro. Kuna taarifa zilizo sambaa kwamba hajapigwa risasi si za kweli, Matukio blog ilipata fursa yakumuona Ponda akiwa anaingizwa MOI leo mchana nakuona hali yake.Ponda yuko katika hali mbaya na hapa ni wakati anaingizwa chumba cha matibabu
Jumatano, 7 Agosti 2013
Jumanne, 6 Agosti 2013
RIPOTI YA MAUAJI YA ARUSHA YAVUJA....
HATIMAYE ripoti ya Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora, kuhusu vitendo vya uvunjaji wa haki za
binadamu na mauaji yaliyotokea Arusha Januari 5, 2011 kwenye maandamano
ya CHADEMA imevuja.
Licha ya ripoti hiyo kufichwa kwa kutosomwa hadharani kwenye vyombo vya habari kutokana na kulishutumu moja kwa moja Jeshi la Polisi, Tanzania Daima imefanikiwa kuinasa.
Licha ya ripoti hiyo kufichwa kwa kutosomwa hadharani kwenye vyombo vya habari kutokana na kulishutumu moja kwa moja Jeshi la Polisi, Tanzania Daima imefanikiwa kuinasa.
Jumatatu, 5 Agosti 2013
MKE WA MTU ALA KIPIGO AKIIBA NGUO KARIAKOO
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)