Alhamisi, 11 Julai 2013

WEMA AKIMBIA NYUMBA BAADA YA KUFANYA FUJO HOTELINI

POLISI wapatao sita Jumamosi iliyopita walivamia nyumbani kwa staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu maeneo ya Kijitonyama kwa lengo la kumkamata kufuatia kesi iliyofunguliwa katika Kituo cha Polisi Kawe jijini Dar.


Awali taarifa zilidai kuwa, tuhuma zinazomkabili staa huyo asiyekaukiwa na matukio ni za kumtukana na kumpiga vibao Godluck Kuyumbu ambaye ni meneja wa hoteli moja maarufu jijini Dar.


Baada ya kesi hiyo yenye jalada KW/RB5988/2013 SHAMBULIO kufunguliwa kituoni hapo Julai 6, mwaka huu mishale ya saa 5 asubuhi, maafande hao wakiwemo wa kike wawili wakiwa wamevaa kiraia walifika mtaa anaoishi staa huyo na kuufunga kabla ya kwenda kugonga katika geti la nyumba yake.
Mara baada ya kugonga geti hilo, alitoka mwanaume aliyefahamika kwa jina la Petman, alipoulizwa kuhusu Wema, alijiumauma huku kijasho kikimtoka kabla ya kutoa jibu la kwamba hakuwepo.
Majibu hayo hayakuwaridhisha polisi hao ambapo walilazimika kuzuia kila gari lililokuwa linatoka


Hata hivyo, hawakufanikiwa kumuona ndipo walipolazimika kumuita mjumbe wa eneo hilo na kuomba ruhusa ya kuingia ndani kufanya upekuzi lakini hawakumtia mikononi na taarifa zikawa mwanadada huyo yuko Zanzibar.

Maafande hao waliomba namba ya simu ya Wema na walipompigia alisema yuko Zanzibar, kesi hiyo anaijua na atakaporejea atajisalimisha mwenyewe polisi.