Ijumaa, 23 Agosti 2013

JE ULIKUWA UNAYAJUA HAYA KUHUSU KANUMBA

Leo kupitia kwa mwanadada Yobnesh Yussuph almaarufu kama Batuli tumeweza kupata jambo moja ambalo watu wengi watakuwa hawajawai kulisikia kuhusu marehemu Steven kanumba.
Mwanadada huyo leo alienda kutembelea kituo kimoja cha watoto yatima kilichopo huku maeneo ya Bunju jijiji Dar es Salaam. 
Merehemu Steven Kanumba alikuwa ni mmoja wa walezi wa kituo cha watoto yatima kimoja kilichopo huko  bunju chenye Zaidi ya watoto (92) wakiwema wa kike (40)  wa kiume hamsini na mbili (52). Kituo hiki kilianzishwa mwaka 2000 kikiwa na watoto wawili na kusajiliwa rasmi mwaka 2006 na kipo chini ya usimamizi wa dada Halima mseta.
Mlezi wa kituo hicho alisema wakati akizungumza na bongomovies kuwa marehemu alikuwa ni mtu wa muhimu sana kwa watoto hao kwani kila mara hakusita kutoa msaada pale ulipohitajika.
Kwa yeyote ambaye angependa kuwasiliana Zaidi na mama mlezi wa kituo hichi basi unaweza kufanya hivyo kupitia namba za simu zifuatazo
0712 720022
0782 720022
0753 720022