Jumanne, 6 Agosti 2013

KUTANA NA VAILET MAMA WA WATOTO 2 ALIYEKIMBIWA NA BABA WA WATOTO WAKE KUTOKANA NA ULEMAVU

Mama Vailet Nyamanga (41) akiwa na Mtoto wake Rose Nyamanga (9) wakikatiza katikati ya mitaa ya Nkuhungu Wilaya ya Dodoma Mjini katika Mkoa wa Dodoma, hivi karibuni. Rose ni mwanafunzi wa darasa la pili katika shule msingi Nkuhugu, Mama huyu, Vailet, ambaye ni mlemavu wa viungo mwenye urefu wa futi mbili, Anaishi
kwa kutegemea msaada kutoka kwa wasambaliwema ambapo kwa siku anaweza kujipatia sh. 2000 hadi sh. 4000.
Na mwanawe Rose ndiye hasa msaada mkubwa kwa mama yake ambaye humuongoza pindi wanapokuwa barabarani katika safari zao za kutafuta riziki na pia ndiye humuhudumia mama yake kwa kumsafisha pindi anapokuwa amejisaidia na pia humlisha  chakula na kumuogesha na kumvarisha nguo.
Rose alianza kumhudumia mama yaketangu akiwa na umri wa miaka (5).  
Mama huyo hadi sasa ana watoto wawili Rose akiwa ni wapili kuzaliwa wa kwanza ni wa kiume ambaye ana umri wa miaka (19), anayeitwa Cristopher Nyamanga, ambapo watoto wote alijifungua kwa kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, lakini hadi sasa baba wa watoto hao hawajulikani walipo baada ya kumkimbia baada ya kupata ujauzito.