MEZA
 kuu ya Majaji walioshiriki katika Usaili ya kutafuta Models 
watakaoshiriki kwenye Ally Rehmtullah 2014 Collection Fashion show 
kutoka kushoto ni Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen 
nchini, Alfred Minja, Ally Hassan, Mrembo na mwigizaji maarufu nchini 
Wema Sepetu, Mwandaaji wa Onyesho hilo ambaye pia ni Mbunifu wa Mavazi 
nchini Ally Rehmtullah, Mwanamitindo Jamillah Nyangasa, Sarah Raqey.
Mwanamitindo maarufu hapa nchini Ally Rehmtullah amefanya maandalizi ya awali ya fashion show yake itayofanyika 30th
 August mwaka huu katika Hoteli ya Serena ambapo zaidi ya wanamitindo 30
 wasichana na wavulana watashiriki katika maonyesho hayo kabambe.
Akizungumza 
na Mwandishi wa habari hizi kwenye mahojiano maalum Rehmtullah amesema 
kwenye onyesho la mwaka huu wasichana watashiriki 20 na wavulana 10 
ambao watavaa mavazi mbalimbali yaliotengezwa na kubuniwa na Rehmtullah 
mwenyewe kwa kuzingatia mila na desturi za Kiafrika.
Katika mchujo
 huo majaji watano watashiriki kuchagua warembo wenye mvuto, kujiamini 
na wenye kuwa na muonekano mzuri kwenye jukwaa ili kuwavutia wageni 
waalikwa ambao watakuwa ni wabunge, mawaziri na viongozi mbalimbali. 
Rehmtullah alilisitiza mwaka huu kwamba onyesho la mitindo ya mavazi 
yatafana baada ya kudhamini wa makampuni kadhaa makubwa hapa nchini.

Pichani juu
 na chini ni Models wa kike wakipita mbele ya majaji wakati wa Audition 
ya kutafuta washiriki watakaonyesha mavazi kwenye Onyesho la Mavazi la 
Ally Rehmtullah 2014 Collection.



Pichani juu
 na chini ni Models wa kiume wakipita mbele ya majaji kwa ajili ya 
kuchaguliwa kushiriki kwenye Ally Rehmtullah 2014 Collection Fashion 
Show.



