Wema Isaac 
Sepetu na Irene Pancras Uwoya kufuatia kuanzisha vipindi vya runinga kwa
 mpigo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Clouds Media Group, 
Ruge Mutahaba, katika harakati za vipindi hivyo, alianza Wema kwa 
kuanzisha ‘aidia’ ya kipindi kipya kiitwacho In My Shoes ambacho 
kitaanza kuoneshwa kuanzia Alhamisi hii, saa tatu na nusu usiku kupitia 
Clouds TV.
Alisema baada ya Wema kutengeneza kipindi hicho na kupata maoni mengi, 
Uwoya akajibu mapigo kwa kuanzisha cha kwake kinachoitwa Paradise 
ambacho kitakwenda hewani Jumanne hii (kesho).
“Mashabiki wa Clouds 
TV watapata kuona vita ya kibiashara, Uwoya atakuwa akionekana katika 
kipindi hicho ambacho kitakuwa kinahusu upakaji rangi katika nyumba za 
watu mbalimbali huku Wema naye akikimbiza katika In My Shoes,” alisema 
Ruge. 
