Kituo cha Sheria na Utetezi wa Haki za 
Binadamu (LHRC) na Chama Cha Wanasheria Tanzanyika vimefungua kesi ya 
Kikatiba katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, vikiomba mahakama 
hiyo itoe tafsiri za kisheria katika baadhi ya Ibara.
Kesi hiyo ya Kikatiba ambayo imepewa 
namba 24 ya mwaka huu, na ambayo bado haijapangiwa jaji, wadaiwa ni 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Taasisi hizo ambazo zinatetewa na 
mawakili wa kujitegemea Harold Sungusia, Francis Stolla na wengine 17, 
kwa mujibu wa hati yao ya madai, walalamikaji hao wamewasilisha jumla ya
 maombi mawili ambayo wanaomba mahakama itoe tafsiri ya kisheria katika 
Ibara hizo kwa kuwa wamewasilisha kesi hiyo ya Kikatiba chini ya sehemu 
ya Tatu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ya mwaka 1977, 
ambayo 
inaainisha  Haki na Wajibu Muhimu.
Wakili Sungusia alilitaja ombi la kwanza
 kuwa, wanaiomba mahakama hiyo itamke kuwa ibara ya 100(1) ya Katiba ya 
nchi inayotoa  uhuru wa majadiliano kwa wabunge wawapo ndani ya bunge 
ambayo inasomeka hivi: “kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na 
utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo 
chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katikaMahakama au mahali 
penginepo nje ya Bunge.”
Wakili Sungusia anadai kuwa Ibara hiyo 
ina ubaguzi ndani yake kwani inayoa uhuru kwa mbunge kujadili ndani ya 
bunge na wakati anajadili jambo hata kama amevunja haki za mtu mwingine 
hataweza kushitakiwa wala kuhojiwa jambo ambalo anadai linakinzana na 
Ibara ya 13(2) ya Katiba ambapo Ibara hii inasomeka hivi; “ Ni marufuku 
kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya 
Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa
 taathira yake’.
‘...sisi tunaomba mahakama itamke wazi 
kuwa Ibara ya 100(1) inakwenda kinyume na matakwa ya Ibara 13(2). 
Zinakinzana, kwa kuwa ibara ya 100(1) ya Katiba inatoa haki tu kwa 
upande wa mmoja wa  wabunge uhuru wao kutohojiwa na inawanyima haki ya 
kuwahoji au kuwashitakiwa wabunge wanaotoa kauli zao bungeni hata kama 
kauli hizo za wabunge zimevunja haki za wananchi,”alidai wakili 
Sungusia.
Wakili Sungusia alilitaja dai la pili 
kuwa ni kuiomba mahakama hiyo itamke kuwa kauli ya Waziri Mku, Pinda 
ambayo ililitaka Jeshi la Polisi kuwapiga wale wote wanaokiuka amri za 
jeshi hilo, kama kauli hiyo nayo inalindwa na kinga iliyowekwa katika 
Ibara ya Ibara ya 100(2) ya Katiba ya nchi ambayo inasomeka hivi: ‘Bila 
 ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote 
inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai 
mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya  ndani ya 
Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au 
vinginevyo.’
Katiba mkutano wa bunge uliomalizika 
hivi karibuni , Waziri Mkuu Pinda akiwa ndani ya bunge aliliagiza jeshi 
la polisi kuwapiga wale wote wanaokaidi amri za jeshi hilo, kwasababu 
serikali imeshachoshwa na vitendo vya baadhi ya wananchi wanaokaidi kwa 
makusudi amri za jeshi la polisi , kauli iliyoleta mhemko kwa jamii huku
 wengine wakiipinga utekelezaji wa agizo hilo na wengine wakiunga mkono,
 hali iliyosababisha LHRC  hivi karibuni  ilizungumza na waandishi wa 
habari wakimtaka Pinda afute kauli yake hiyo ama sivyo watamfikisha 
mahakamani.
