Ijumaa, 23 Agosti 2013

BODI YA UKAGUZI YAIPIGA STOP MOVIE YA FOOLISH AGE YA LULU


Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza nchini imeipiga stop filamu ya Foolish age ya msanii wa kike mwenye mvuto Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kukuta picha zilizo nje ya maadili ya Kitanzania katika filamu hiyo, filamu hiyo ambayo ilipanga kuzinduliwa mwezi huu tarehe 30 katika ukumbi wa Mlimani City inahitaji marekebisho.


Kikwazo kilichoikumba filamu hiyo ni nguo fupi zilizotumika katika waigizaji walioshiriki katika filamu hiyo ambayo inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la filamu Bongo kama itafanikiwa kuzinduliwa na kuingia sokoni, juhudi zinafanyika kuhakikisha kuwa marekebisho yanafanyika ili kwenda na ratiba kama ilivyopangwa.

Hivi sasa baada ya urasimishaji wa filamu mamlaka na taasisi zinazohusika na masuala ya filamu zimekuwa makini na kuhakikisha kuwa filamu zinazoingia sokoni na zile zinazozinduliwa kukaguliwa kabla ya kufanyika kwa matukio hayo kama ilivyokuwa awali, kama filamu hiyo ya Foolish age itashindwa vigezo vya madaraja yanayotolewa na Bodi hiyo haitaonyeshwa.

Lulu ndio mwigizaji bora wa kike kwa mwaka 2013 kupitia tamasha la filamu la kimataifa la ZIFF katika kipengere cha tuzo za Bongo movie kilichopewa jina la Zuku Bongo movie Awards zilizotolewa katika ukumbi wa Ngome Kongwe.