Ijumaa, 23 Agosti 2013

MADAM RITA ASEMA KUWA NAY WA MITEGO NI MBUNIFU NA ANAMKARIBISHA KUFANYA SHOW KWENYE BSS

Rita Paulsen hana mpango wa kumshtaki Nay wa Mitego kwa kuichafua Bongo Star Search kwenye Salam Zao. Infact aliusikia wimbo huo hata kabla ya haujatoka.
1185959_596418857075506_439036066_n
Madam Rita alikuwa akiongea kwenye U Heard ya Clouds FM leo ambapo amezikanusha tetesi zilizopo mtaani kuwa amemfungulia kesi ya ‘defamation’ Nay kutokana na kuzusha kwenye wimbo huo kuwa washindi huwa hawalipwi fedha zote.
“Hata muda wa kuongelea hicho kitu naona ni wastage of time. He is not worth my time,” alisema Rita.
Hata hivyo, Madam Rita amesema Nay ni mbunifu na ametumia fursa hiyo kuimba wimbo uliokuwa gumzo baada ya kutoka.
“He is creative, big up to him, very creative you man.” Amesema hana tatizo kama Nay akiperform kwenye show hiyo na hata kama akiuimba wimbo huo.