Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene leo jijini Dar es
Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa
Idara hiyo amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa “twitter ”
na wanyarwanda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal
Havyarimana.
“Taarifa hizi haina ukweli wowote na
zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete,” amesema Mwambene
na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na
kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na
ukweli wowote.
Madai hayo yaliandikwa jana na
mitandao ya Rwanda wakidai kuwa mama Salma Kikwete ni
Mnyarwanda na ni binamu wa aliyekuwa rais wa zamani wa
Rwanda.