Hatimaye Sheikh Ponda Issa Ponda leo majira ya saa nn Asubuhi amepelekwa katika Gereza la Segerea.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyekuwepo
eneo la tukio ameipasha munirablog kwamba ilipofika majira ya saa nne
Asubuhi walikuja Maaskari na kumchukuwa Sheikh Ponda na kumpeleka
Gerezani Segerea.
,"Aah wamekuja Maaskari wengi
wakatufukuza fukuza wakaingia wodini wakaongea na Daktari
wake,wakaandika andika kisha wakamchukuwa na majeraha yake,wala
usisumbuke kuja kumuona,hapa hayupo yupo Segerea",alisema mpashaji wa
habari hizi.
Sheikh Ponda alifikishwa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa (MOI) siku ya Jumamosi ya tarehe
10/08/2013 Saa saba mchana kwa ajili ya matibabu akitokea mkoani
Morogoro baada ya kupigwa Risasi na wanao adaiwa kuwa ni polisi,lakini
Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro
limekanusha madai hayo.