Kuna tofauti kubwa kati ya mabinti wa UDSM na wale wa UDOM. Mbali na 
kwamba wote ni wazuri na wamemeenda vidato lakini zipo tofauti kubwa 
baina yao zinazowatofautisha. Kwa ujumla tofauti zao ni hivi zifuatazo;
Muonekano (image)
Binti wa UDSM mara nyingi atapenda avae vitu mpaka aonekane kama 
mwanamitindo. Atajiwekea make up za kila aiana japokuwa tayari ana uzuri
 natural. Atataka avae fasheni mpya mpya zinazotokana kwa kuwa yuko town
 na mara nyingi hata kama boom haliruhusu kuna wananchi wengi wa 
kuwapiga mizinga.  Nguo zao wananunulia Mlimani City, Quality Center, 
Makumbusho, Mwenge kwa White na maeneo mengine kama hayo.  Jinsi 
wanavyovyaa unaweza ukawaogopa kudhani ni expensive saaaaana.
Binti wa UDOM kwa upande mwingine anavaa kawaida tu. Viatu vyake vya 
mchomekeo wanavinunua pale SabaSaba lakini waulize wavulana UDOM sasa, 
watakwambia binti katoka bomba yule si mchezo. Viatu vyao ni bei za 
kawaida na huvumilia hali zote za hewa. Huwa shopping zao wanafanya Saba
 Saba.
Sehemu ya kuangalia movie (cinema)
UDSM huwezi kumpeleka binti kucheka movie room kwako! Sijui eti Hall 3
 au ghetto Survey! Utampeleka Suncrest Quality Center au Mlimani City na
 hapo uweke bajeti ya PopCon na mazagazaga kibao ya kucheki cinema.
Binti wa UDOM wewe tu na laptop yako unamkaribisha chumbani Block 9, 
10, etc maeneo ya Haiti mnacheki movie huku mkinywa maji ya kudownload, 
bites za Discount shop au chai. Umemaliza.
Sehemu ya kukutania (Date location)
Kama unadhani binti wa UDSM utampeleke room yako namba 2409 kule Hall
 3 sahau! Kama huna ghetto la ukweli Survey au Sinza au Ubungo Maziwa au
 unamiliki nyumba kabisa jua imekula kwako. Sehemu ya kukutania lazima 
iwe ya kueleweka na treatment isomeke vizuri kama misosi iliyosimama, 
Pizza, Burger, Chicken Chips, etc. Hapo lazima Bamaga upajue vizuri, 
Mikocheni na Sinza. Kishushio Savanna au Red Bull. Mjomba huna hivyo 
UDSM utawapata wa kuhesabu kukusikiliza maelezo yako ya kuunga unga.
Binti wa UDOM yeye hata hajali. Wewe tu, uwe kule porini mnapaita 
Ng’ox au Social Room kwako atakuja. Mtengenezee chai kwa ule mkate wako 
wa juzi halafu anza kumwaga point zako. Huna haja ya kupajua Area D, 
Area C wala Lodge za Area A ila ukikosea ukakuta mwenye kaupepo ka jiji 
lazima kuku wa Club Maisha na 84 ujue bei yake.
Upatikanaji wao (Availability)
Binti wa UDSM atakuona akitaka kukuona si kinyume chake. Ukimpigia 
simu mkutane atakupa sababu kibao utabaki kichwa kinakuuma ila yeye 
akikupigia simu mkutane hataki kusikia sababu yako hata moja. Anapenda 
yeye awe na control.
Binti wa UDOM yeye anaelewa principle ya give and take vizuri sana. 
Anaelewa mla lazima aliwe na anaelewa ili uhusiano uwepo lazima kila mtu
 aplay part yake.  Ukimpigia simu baada ya dakika au saa chache utamuona
 na wanapenda kutembea na wavulana wao campus. Kama unabisha angalia 
idadi ya mabinti wa UDSM wanaotembea na boys ndani ya campus na wale wa 
UDOM wanaofanya hivyo ndani ya campus.
Mtazamo wao kuhusu mapenzi (Perception of love)
Binti wa UDSM atakupenda kwa ile ulichona nacho. Kichwa class, una hela au famous. Nje ya hapo ni wa kuhesabu bro.
Binti wa UDOM atakupenda jinsi ulivyo hasa kama shule kasoma Songea 
huko kwao vijijini chuo katua Dodoma, ila ukikuta ana kahewa ka Dar 
kidogo lazima utasanda. 
